-
1. Ekaristi Takatifu
Uongozi wa Parokia ya Mt. Monica Buhongwa unapenda kutoa shukrani za dhati kwa waumini wote waliojitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Ekaristi Takatifu, na hivyo kuyafanya maadhimisho hayo kuwa ya kipekee, yenye heshima na mafanikio makubwa.
Kwa namna ya pekee, tunatoa pongezi na shukrani kwa Baba Paroko pamoja na Paroko Mwenza kwa uongozi wao mzuri, ushirikiano na juhudi kubwa walizozifanya kuhakikisha maadhimisho haya yanakuwa ya kuvutia na yenye baraka nyingi kwa jumuiya nzima ya waamini.
Pia tunawapongeza kwa dhati wajumbe wote wa Kamati ya Maandalizi ya Ekaristi Takatifu kwa kujitoa kwao, mipango mizuri na kazi kubwa waliyoifanya hadi kufanikisha tukio hili muhimu katika maisha ya Kanisa letu.
Shukrani za pekee ziende kwa vyama vyote vya kitume, hususan WAWATA, VIWAWA na UWAKA, kwa maandalizi mazuri ya mabanda na namna walivyoshiriki kwa uchaji na furaha katika kumpokea Yesu Kristo aliye hai katika Sakramenti ya Ekaristi Takatifu.
Vilevile, tunawapongeza viongozi na waumini wa kanda zote kwa moyo wao wa ukarimu na imani, kwa kuandaa na kuwasilisha zawadi mbalimbali kwa Yesu wa Ekaristi Takatifu kama ishara ya upendo, shukrani na sadaka kwa Mungu.
Mwisho, tunatoa pongezi nyingi zaidi kwa waumini wote kwa moyo wenu wa ibada, uchaji wa Mungu na ushiriki wenu kamili katika sherehe hizi takatifu za kumtukuza na kumwabudu Yesu Kristo katika Ekaristi Takatifu.
Mwenyezi Mungu awabariki nyote, azidi kuimarisha umoja wetu, na kutujalia neema ya kuendelea kumshuhudia Kristo katika maisha yetu ya kila siku.
"Asanteni sana kwa ushirikiano wenu na Mungu awabariki."
-
1. DOMINIKA YA 26 YA MWAKA C
JUMUIYA YA ZAMU WIKI IJAYO
Jumuiya ya zamu wiki ijayo ni jumuiya ya Mt. andrea Mtume na Mt. bikira Maria Maria Mama Wa Fatima.
Jumuiya zifuatazo Mnaombwa mjiandae
- Mt. Filomena na Mt. Kaloli Lwanga
- Mt. Petro na Mt. Ritha
- Mt. Maria Consolata na Mt. Maria Goreth
-
1.
-
2.
-
1.
-
1. hhaha
-
2. hhaha
-
3. Tangazo la ndoa
-
4. 1 Maombi ya Jioni Evening Devotion
-
5. 2 Mafunzo ya Ndoa na Sakramenti ya Kipaimara
-
6. 3 Misa ya Watoto
-
7. 4 Siku ya Matendo ya Huruma
-
8. 5 Harambee ya Ukarabati wa Kanisa
-
9. Hitimisho